UJENZI WA JENGO LA PIUMA.

Hii ni taarifa ya ujenzi kwenye Jengo la PIUMA, tunashushukuru kwa misaada ya wafadhili na marafiki wote wa PIUMA kwa michango yenu mnayotoa kwa ajili ya kuisaidia PIUMA kwa mambo mbalimbali.
Mpaka sasa jengo letu la PIUMA vyumba vilivyoisha kusakafiwa ni nane, katika hivi vyumba nane vyumba vine vinaendelea kupigwa dari, vitapakwa rangi na vimefungwa milango tayari. Lakini vyumba vingine vilivyobaki hatuna fedha kwa ajili ya kuendelea na ujenzi, hivyo basi mpaka sasa ujenzi umesimama.
Endapo tutapata msaada wa fedha tutaendelea na kusakafia chumba kikubwa cha katikati, veranda na ukarabati wa vitu vingine.
Pamoja na nguvu kazi za wanachama bado tunahitaji msaada wa fedha kwa ajili ya kuweza kukamilisha zoezi hili.
Malengo yetu tulipanga kuwa endapo tutamaliza jengo haraka mwezi wa tisa mwaka huu tuwe tumeshahamisha ofisi kwenye jengo letu la PIUMA.

Ahsante.