TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA PIUMA.

Sasa wanachama wa PIUMA wameamua kuanzisha timu ya mpira wa miguu ili kupima afya zao. Timu hii imeshaanza mazoezi taraya kwa ajili ya kujipima afya na wanataka kuanza kushindana na mashirika mengine ya watu wanaoishi na VVU.

Timu hii ni ya mchanganyiko wanawake kwa wanaume , waliopima afya zao na ambao ni wanachama wa PIUMA. Tayari wameshapata barua ya mashindano ya ujirani mwema kutoka shirika la watu wanaoishi na VVU MASUPHA.

Baadhi ya wanachama wameshaanza mazoezi tayari kwa ajili ya kwenda kushindana na shirika hili la MASUPHA Makete tarehe 13/7/2008.

Na siku ya mashindano haya itakuwa ni siku ya uzinduzi wa KUZUIA MAAMBUKIZI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO (P.M.T.C.T) ambayo yatafanyika tarehe tajwa hapo juu.

Tumepewa mipira miwili na Gabe kwa ajili ya kufanyia mazoezi.

Hao hapo juu ni baadhi ya wanachama walioanza mazoezi.