RIPOTI YA SAFARI YA ARUSHA.
Tumeondoka Bulongwa tarehe 27/7/2008 tumefika Arusha tarehe 29/6/2008.
Tumefika Arusha 4:30, tumepokelewa na ndugu Jackson Mbogela.
Tumetafuta gesti mahali pa kupumzika.
Tumekaa kwa pamoja na kuandika barua ya kwenda Polisi na kwa mkuu wa
Mkutano na kopi kwa ofisi kuu ya Arusha kwa ajili ya kuomba kushiriki
Mkutano, na hapo hatukujua mkutano unafanyika sehemu gani mjini Arusha.
Tulitafuta magazeti ya dini toleo la tarehe 28/6/2008, tulipata gazeti
zuri sana ambalo lilitufahamisha mkutano ulipo ACC 8:30. Tulikwenda
polisi tulipokelewa vizuri na Polisi wa pale na akatupeleka kwa mkuu
wa Upelelezi, tulimpa barua yetu akaisoma tukamweleza lengo kuu
tulilokuja kwenye mkutano, tuliulizwa tuko wangapi, tulimjibu kuwa
tupo watano, kwa kweli mkuu wa upelelezi alitusaidia sana mawazo, na
muda gani wa kuingia kwenye ukumbi wa mkutano.
Tulipokwenda kwenye kituo cha polisi saa 10:12 tukaenda ofisi kuu za
KKKT tulikuta hawapo. Tukaenda sehemu ambayo mkutano unafanyika (AICC)
tukaambiwa leo ni jumapili ofisi zimefungwa, tuliondoka saa 12:30
kwenda kupumzika kujiandaa kwa ajili ya kazi ya kesho.
Tarehe 30/6/2008 tuliamka saa 12:30 kwenda ofisi kuu ya KKKT tumefika
1:20 tumeona bado hazijafunguliwa. Baada ya hapo tumeondoka kwenda
AICC ambako mkutano unafanyika tulifika AICC saa 2:7 tulimwona mama
mmoja kwenye chumba cha mapokezi tukamwambia tunashida na mkuu wa
Mkutano yaani KATIBU tunaomba kuruhusiwa kuingia kumwona Katibu.
Tulichekiwa kama tuna vitu vya hatari, tuliruhusiwa kwenda kumwona
Katibu wa Mkutano, tulisindikizwa na huyo mama wa mapokezi,
tukapokelewa vizuri, tukamweleza kwa kifupi kazi tuliyojia kutoka
Makete, alipokea barua yetu na kwenda kumkabidhi mwenyekiti wa
mkutano, tulipanda wote lifti kwenda gorofa ya saba ambapo tuliambiwa
tusubiri sehemu ya chai tulitoka saa 5:00. alitokea mama mmojas ambaye
ni mjumbe wa mkutano alikuja na mbwembwe zake alitaka tutoke lakini
tulisimama ngangali hatukumsikiliza, ndipo walipotoka kunywa chai
tulisimama na mabango yetu huku tumevaa tisheti za PIUMA tatu, mpya
moja na mbili za zamani. Mabango yote yaliandikwa kwa kiingereza,
Mabango yalisema hivi.
(i) Donor Money stolen from Makete must be returned (Pesa ya wafadhili
iliyoibiwa Makete irudishwe)
(ii) Corruption lack of account ability lack of Transparencey of the
ELCT/SCD quietness of donors, kills HIV + Makete ( Ufisadi, ukosefu wa
uwajibikaji, ukosefu wa uwazi wa KKKT/DKK ukimya wa wafadhiri unauwa
wa (VVU) Makete.
(iii) Ice is melting on Mt. Kilimanjaro PLWHI lives are perishing in
Makete due to corruption (Barafu imeyeyuka mlima Kilimanjaro maisha ya
wa (VVU) yanayeyuka kwa sababu ya UFISADI.
(iv) LWF talk on the on going state of crisis at BLH (Kongamano la
makanisa zungumzeni juu ya mgogoro wa BLH)
Baada ya hapo tulisimama na mabango mbele ya ukumbi muda wa dakika 30
tuliitwa na Katibu wa miradi anayesimamia ukanda wa Afrika, tulikaa
ofisini mwake dakika 45 naye alitutia moyo sana kwa kazi tunayofanya.
Wana PIUMA baada ya hapo tulitoka na kwenda kupata chakula ilikuwa saa
6:15, saa 7:30 tulikwenda redio 5 (five) tulitoa malalamiko yetu
tuliyojia Arusha, saa 8:20 tulikwenda TBC Televisheni huko nako
tuliwaeleza tulilojia Arusha, tukawaeleza yanayo tusibu wana Makete,
tulimaliza kazi saa 10:30 tukarudi kupumzika na kwenda kufuatilia
tiketi.
1/7/2008 tuliondoka Arusha kurudi nyumbani Bulongwa tumefika tarehe 2/7/2008.
Huu ndio mwisho wa ripoti ya safari yetu ya Arusha.
Ahsante.
Wema Sanga.