MWANDISHI WA HABARI OFISINI PIUMA

MWANDISHI WA HABARI OFISINI PIUMA

Mwandishi wa habari Simbeye ambaye alikuja jana tarehe 27/8/2008 katika ofisi ya PIUMA saa 5:30 asubuhi akiwa ametokea DSM.

Mwandishi huyu alisema kuwa amekuja kujua historia fupi ya PIUMA.

Kwa bahati mbaya Katibu Wema Sanga hakufika ofisini, lakini alibahatika kuonana na baadhi ya wanachama kama, John Nyihava, Amini Pilla na Apolo Mbogela.

John Nyivaha alieleza kwa kifupi historia ya PIUMA, alisema kuwa PIUMA ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na wanachama 5, ambao ni Kabuyu Kyando ambaye ni Mwenyekiti wa PIUMA, Wema Sanga ambaye kwa sasa ni msaidizi wa Katibu Mkuu wa PIUMA, Bernadi Kyando, Herode Fungo, Rehema Nyamule.

Aliendelea kusema kuwa shughuli ambazo zinafanywa na PIUMA ni HBC, VCT , Mobile VCT, ushauri wa lishe kwa wanaotumia dawa za kupunguza makali ya VVU ,pamoja na kutoa ushauri juu ya magonjwa ya zinaa.

Mwandishi aliuza habari za HBC, VCT na Mobile VCT.

Juma Nzige (Mganga) alisema kuwa huduma za HBC zinafanywa na wanachama waPIUMA .

Aliendelea kusema kuwa Kituo cha VCT kilisimamishwa tangu mwezi waPili 2008 baada ya Nesi aliyekuwa anafanya kazi PIUMA mkataba wake kuisha .

Baada ya hapo viongozi wa PIUMA waliandika barua ya kuomba manesi kutoka Bulongwa Hospitali kwa ajili ya kuendelea kutusaidia kazi hii. BLH walitukubalia ombi letu na kutupa manesi wawili ambao walikuwa wanafanya kazi kwa kubadilishana, manesi hawa walifanya kazi kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu, ndipo tulipopata barua kutoka BLH ya kusitisha manesi wao kutoa huduma katika Kituo chetu na kusema kumekuwa na uhaba wa manesi katika Hospitali yao.

Hapo ndipo Uongozi wa Afya wa Wilaya ulipokuja kufunga kituo chetu na kusema kuwa kituo kitafunguliwa mpaka mtakapoajiri manesi wenu.

Baada ya hapo uongozi wa PIUMA uliwasilisha taarifa hii kwa wafadhili wao, ndipo wafadhili walipochukua jukumu la kuajiri Nesi Potania Mfuse na Mganga Juma Nzige.

Watumishi hawa waliwasili katika ofisi ya PIUMA na uongozi wa PIUMA uliwapeleka ngazi zote za serikali pamoja na uongozi wa Afya kwa ajili ya utambulisho.

Baada ya hapo Uongozi Afya wa Wilaya Makete ulisema kuwa PIUMA tunatakiwa kusajiri upya kituo cha VCT, viongozi wa PIUMA pamoja na wafadhili wao walifanya kazi hio na kufanikiwa kusajiri kituo.

Baada ya kurudi kutoka kusajiri kituo viongozi w PIUMA walienda kwa viongozi wa Afya wa Wilaya kupeleka ripoti ya kusajiri kituo, hapo ndipo viongozi hawa walipogundua kitu kingine, walisema kuwa wahudumu wetu hawajapitia mafunzo ya VCT COUNSELOR," kweli hapo ndipo kazi ilipoanza", Viongozi wa PIUMA hawakukata tamaa, waliwasiliana na wafadhili wao na kuwaeleza hili, wafadhili walikubaliana nalo na kuwaambia kuwa yafanyike mawasiliano ili kupata sehemu ya kuweza kupata mafunzo, mawasilano yalipofanyika mafunzo yalipatikana AMREF na kusema kuwa wanatakiwa kuanza mafunzo mwezi wa Nane.

Lakini cha kusikitisha ilipofika mwezi wa nane DACC wa Wilaya Makete alisema kuwa mafunzo yamesimamishwa kwa sababu AMREF wanapitia mwongozo wa mafunzo ili kuufanyia marekebisho. Tarehe itatangazwa upya ya kuanza mafunzo.

Hatukukata tamaa,Tuliendelea kuwafuatilia kila wiki, tulifanya hivyo mwezi mzima. tulipoenda kwa mara ya mwisho kuwaambia kuwa Wafadhili wameamua kuja kufunga kituo chao mwezi wa kumi, hapo ndipo waliposema kuwa watatuazima nesi ambaye tutakuwa tunafanya nae kazi, na nesi huyu tutatakiwa kumlipa kwa siku sh. 20,000/= kiasi ambacho kitaliathiri shirika pamoja na wafadhili wenyewe.

Baada ya hapo Mwandishi aliomba kukiona kituo chetu cha VCT.

Hapo ndipo walipoondoka na Juma kuelekea kwenye kituo cha VCT, huko walienda kuonana na Nesi Potania Mfuse.

Mwisho mwandishi alipewa Nakala ya Ripoti ya Mobile VCT tulivyopima mwaka jana.

Ni hayo tu.

Visit PIUMA's website at www.piuma-simba.org