KIKAO CHA KAMATI ZOTE ZA PIUMA KILICHOFANYIKA TAREHE 25/06/2008

UTANGULIZI: Kikao cha kamati zote za PIUMA kimefanyika jana tarehe tajwa hapo juu kwa ajili ya kuwaelimishwa wajumbe wa kamati kujua wajibu wa kazi kwa kila kamati, kikao kilifunguliwa saa 4:00 asubuhi.
Mwenyekiti aliwaeleza wajumbe kuwa tumetembelewa na mgeni toka Canada ambaye amekuja kututembelea, na mgeni huyu amekuja na vifaa vifuatavyo.
- Compyuta, kamera na begi ya compyuta.
Mwenyekiti aliwaeleza kuwa mgeni huyu amekuja kufungua website ya PIUMA, kuwatembelea wanachama wa PIUMA pamoja na vikundi vyake. Ametumwa na Royal kuja kufanya kazi nasi, atakuwepo kwa mwezi mzima.
Alimkaribisha mgeni ili ajitambulishe, mgeni alisema kuwa yeye anaitwa Gabe Maldoff. Wajumbe walishukuru kwa ujio wake huyu mgeni na kumpokea kwa kuimba wimbo wa PIUMA.
Wajumbe waliokuwa wamehudhuria walikuwa 28 kati ya wajumbe 41 katika kamati zote, katibu Mkuu wa PIUMA aliwasomea wajumbe wajibu wa kila kamati.
1. KAMATI YA UTENDAJI
Kamati hii ndio kamati kuu itawajibika na mambo yote yanayohusu mambo yote ya PIUMA pamoja na kuwajibisha kamati ndogondogo na viongozi wa PIUMA.
2. KAMATI YA FEDHA
Kamati hii itawajibika na mabo ya fedha za PIUMA, kuandaa bajeti, kuandaa ripoti, kudhibiti pesa, na mambo yote yahusuyo fedha.
Kamati zingine zote zitawajibika kwa kufuata wajibu wa kila kamati na kamati hizi zitapeleka maombi na maazimio yao kwenye kamati ya utendaji na kamati hii ndio yenye kutoa uamuzi wa mwisho.
Mwisho kikao kiliahirishwa kwa kuimba nyimbo za PIUMA. Kikao kiliahirishwa saa 8:00 mchana.